karibu kwenye kipengere hiki kujifunza elimu kuhusu mzunguko wako wa hedhi kila siku. Wanawake wengi wanashindwa kutambua na kutofautisha mzunguko wa hedhi na kuwa kwenye hedhi. Ambapo hili ni swali nililokuwa nikiulizwa na wanawake wengi.
Kwa hio makala hii inalenga kutoa elimu juu ja jambo hili na pia itamuwezesha mwanamke kuzifahamu siku zake za hatari na siku zisizo za hatari kwenye kushika mimba.
JE, MZUNGUKO WA HEDHI NI NINI?.
Huuu ni mzunguko unaotokea kwa mwanamke baada ya kufikisha barehe na kukoma baada ya kufikia uzee (miaka 45-50). Tunauita mzunguko wa mwezi kwani hutokea ndani ya siku 28 kwa wanawake wengi na kujirudia tena. Pia kuna baadhi ya wanawake ambao mizunguko huchukuwa siku 21 hadi 35 kutokana Na asili ya mtu.
JE, KUWA KWENYE HEDHI NI NINI?.
mwanamke atasemekana yupo kwenye hedhi pale atakapo anza kutokwa damu ukeni. Ambapo wanawake wengi huchukua siku 3 hadi 7 kutokwa na damu kutegemea na asili yake. Mara nyingi kwenye siku hizi mwanamke anaambiwa kuwa yupo mwezini. Kwa kitaalamu kipindi hiki kinaitwa MENSTRUATION (au BLEEDING kwa kiingereza)
JE, SIKU ZA HATARI NI ZIPI.
siku za hatari ni zile siku ambazo mama anakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kushika mimba kama atafanya tendo la ndoa. Tunaziita siku za hatari kwani ndio kipindi ambacho mama analiachia yai kwenda kwenye mirija ya uzazi, ambapo huko yai husubiria mbegu za kiume kwa ajili ya kufanyiwa urutubishaji na kutengeneza kitoto. Siku hii ya ovulation ni siku 1 tu, ambayo hutokeaga siku ya 14 kabla ya kuanza mzunguko mwengine. Kwa hio siku zote zinazozunguka siku hii tunaziita siku za hatari, ambapo huwa ni siku 7 siku 3 kabla ya ovulation, siku 3 baada ya ovulation, na siku yenyewe.
JE, NITAITAMBUAJE SIKU YA OVULATION?.
Kama ulikuwa unatafuta mtoto unaweza kutumia njia hizi kutambua siku ya ovulation, siku ambayo yai linaachiliwa na mama kwenda kwenye mirija ya uzazi kwa ajili ya kusubiria mbegu za baba ili lirutubishwe na kutengeneza kitoto.
1. ANGALIA KALENDA YAKO.
Ovulation huwa inatokea katikati ya mzunguko wako wa kila mwezi (menstrual cycle). Mizunguko ya watu wengi ni siku 28, lakini pia huweza tokea siku 21 mpaka 35 ambapo pia ni kawaida. Hivyo unatakiwa kujua mzunguko wako ni siku ngapi. Sio kila mtu ana siku 28. Wakati mwingine mzunguko wako unaweza kutofautiana kutokana na mambo mbali mbali kama stress, kuchoka, safari, mazoezi. Hivyo unatakiwa kutambua siku zako kwa miezi kadhaa kujuwa mzunguko wako wa kawaida ni upi. BAADA ya kujuwa siku zako hesabu kutokea kutokea nyuma na kutoa kwa 14 ambapo siku utakayo ipata ndio siku yako ya ovulation. kwa mfano kama una siku 30 za mzunguko wako unachukuwa 30 na kutoa 14 unapata 16: hii siku ya 16 ndio siku yako ya ovulation katika mzunguko wako. Lakini kama siku zako huwa haziko kawaida hubadilika mana kwa mara basi ni vizuri kutumia njia nyingine.
2. SIKILIZA MABADILIKO YA MWILI WAKO.
Kama wewe upo kwenye 20% ya wanawake ambao miili yao wanaijuwa kuhusiana na mabadiliko ya aina yoyote basi njia hii inawafaa. kwa mfano Unaweza kusikia maumivu (cramps),mara nyingi upande mmoja. upande ambao yai limeachiliwa, basi ujuwe kuwa upo kwenye ovulation.
3. ANGALIA JOTO LA MWILI WAKO.
Njia hii inaweza fanywa kwa kutumia kipima joto maalum. Ambapo unaweza chukua joto lako asubuhi kabla hujatoka kitandani na kisha ufananishe na joto la siku za kawaida kwani siku ya ovulation joto huwaga ni la juu.
4. FAHAMU MABADILIKO YA SHINGO YA KIZAZI KWENYE UKE WAKO (CERVIX).
Hii ni sehemu ambayo iko kama shingo katikati ya uke na mji wa mimba(uterus), ambapo sehemu hii hutumika kupitisha kichwa cha mtoto mama akiwa anajifungua na inakua chini, ngumu na imejifunga. Wakati ovulation inaanza sehemu hii inajivuta nyuma kidogo, inalainika na inafunguka. Wanawake wanaweza kuzisikia hizi tofauti. Ambapo ukiona tofauti hizi ujuwe upo kwenye ovulation.
5. NUNUA KIFAA KINACHOITWA OVULATION PREDICTOR KIT.
Kama una uwezo au kama zinapatikana sehemu unapoishi kifaa hiki kina uwezo wa kukusaidia kujua siku ambayo upo kwenye ovulation.
JE, NI SIKU GANI SIO ZA HATARI?.
Siku zisizo za hatari ni siku ambazo mwanamke anaweza fanya tendo la ndoa bila kushika ujauzito. Siku ambazo sio za hatari zi siku zote za mzunguko wa mwanamke ukatoa zile siku 7 za hatari.Ambapo baadhi ya wanawake huongeza siku 2 baada na siku 2 kabla kwa ajili ya uhakika zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Rekebisha mzunguko wako wa hedhi kwa vyakula hivi.
SABABU ZA KUBADILIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI. 1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akit...
-
SABABU ZA KUBADILIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI. 1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akit...
-
karibu kwenye kipengere hiki kujifunza elimu kuhusu mzunguko wako wa hedhi kila siku. Wanawake wengi wanashindwa kutambua na kutofautisha ...
No comments:
Post a Comment