SABABU ZA KUBADILIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI.
1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
2. Msongo wa mawazo (stress)
3. Hofu
4. Woga
5. Mabadiliko ya kisikolojia
6. Uvimbe kwenye kizazi
7. Matatizo kwenye mfumo wa homoni
8. Matatizo kwenye vifuko vya mayai
9. Mimba kuharibika
10. Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
11. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
12. Kutokwa na uchafu ukeni
13. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
TUMIA VYAKULA HIVI KUTIBU TATIZO
1. Papai
Papai
Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.
Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.
Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.
2. Mdalasini
Mdalasini
Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.
Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).
• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.
• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.
3. Tangawizi
Tangawizi
Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’. Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa
• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.
• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.
4. KOTIMIRI (Parsley):
Kotimiri
Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii. Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.
Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango. Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.
Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.
5. MREHANI
Mrehani
Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla. Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.
• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.
• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.
• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.
6. MAJI YA KUNYWA
Maji ya kunywa
Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.
Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.
Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.
7. MBEGU ZA MABOGA:
Mbegu za maboga
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote.
Mbegu za maboga zitakusaidia kuweka sawa homoni zako kama hazipo sawa, zitakuondolea msongo wa mawazo (stress) na kukurudishia viinilishe mhimu ambavyo unavitahitaji kwa ajili ya afya yako ya uzazi. Ni nzuri pia kwa yule ambaye amefika ukomo wa siku zake.
Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Rekebisha mzunguko wako wa hedhi kwa vyakula hivi.
SABABU ZA KUBADILIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI. 1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akit...
-
SABABU ZA KUBADILIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI. 1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akit...
-
karibu kwenye kipengere hiki kujifunza elimu kuhusu mzunguko wako wa hedhi kila siku. Wanawake wengi wanashindwa kutambua na kutofautisha ...
No comments:
Post a Comment